Bw.
Peragius Cosmas mwanafunzi aliyehitimu shahada ya Uhasibu na kupata
GPA 4.91 akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha CBE
Prof.Emanuel Mjema.
Bi.
May Issa mwanafunzi aliyehitimu shahada ya kwanza ya Usimamizi wa
manunuzi na kupata GPA 4.92 Akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mkuu
wa Chuo cha CBE Prof.Emanuel Mjema.
Kwa
kile ambacho kimeonekana ni tishio kwa chuo cha Elimu ya Biashara
(CBE) wanafunzi hawa kutoka kampasi ya Dodoma wameweza kupata ufaulu
mkubwa katika masomo yao.
Bi.
May Issa Mwanafunzi aliyehitimu shahada yake ya kwanza ya Usimamizi
wa Manunuzi katika mahafali ya 49 ya chuo cha Elimu ya Biashara CBE
Dodoma mwaka 2014 ametangazwa kuwa mwanafunzi wa kwanza aliyeongoza kwa
ufaulu kwa kupata GPA ya 4.92. ambapo aliweza kupata alama A 28 ,
alama B+ tatu na alama B moja kati ya masomo 32 ya shahada yake
ya kwanza ya Usimamizi wa manunuzi akifuatiwa na Bw. Peragius Cosmas
aliyepata GPA ya 4.91.
Kwa
upande wake Mwanafunzi mwingine Bw, Peragius Cosmas aliye kuwa
akisoma Shahada ya kwanza ya Uhasibu yeye pia alionyesha maajabu kwa
kuweza kupata GPA ya 4.91 ambapo aliweza kupata alama A 29 na
alama B+ tatu kati ya masomo 32 ya shahada yake ya kwanza ya
uhasibu.
Hivi
karibuni katika Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) pia tulishuhudia
Msichana Doreen Kabuche aki ]ongoza kwa ufaulu UDSM kwa kuwa Mhitimu
bora wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2014, Doreen Kabuche
alitangazwa kuwa kinara kwa ufaulu kwa kupata alama A 32 na B+ sita kati
ya masomo 38 ya shahada ya Takwimu Bima (Actuarial Science). Kwa alama
hizo, Doreen alipata wastani wa alama za ufaulu (GPA) 4.8 na kuacha
alama ya 0.2 ili kufikia kiwango cha juu kabisa cha ufaulu cha alama
tano.
PICHA ZAIDI INGIA HAPA
PICHA ZAIDI INGIA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...