Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum liliozunguuka katika uwanja huo leo.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Viongozi wa Kitaifa wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Ankal, ati leo ni sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara au Uhuru wa Tanganyika????

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe mdau hapo juu kwani hujui kama kuna tanzania bara na visiwani ? Hiyo tanganyika ilishafutwa tangu mwaka 64

      Delete
    2. Leo miaka 53 ya uhuru upanga hakuna umeme toka saa tisa mchana sasa ni saa saba usiku
      aiseeeeee ni shider

      Delete
  2. Kwani Zanzibar ilipata uhuru wake mwaka gani? hivi kuna utofauti wa uhuru wa Tanganyika na Zanzibar? kweli tunayatangazia mataifa ujinga kwamba hatuelewi hata historia ya nchi yetu.

    ReplyDelete
  3. Viongozi wa Taifa akiwemo raisi, makamu wa raisi na raisi mtarajiwa.

    ReplyDelete
  4. kwani Tanzania bara ilizaliwa lini jamani au historia imebadilika. tunawachanganya watoto wetu. huu ni uhuru wa TANGANYIKA. sherehe za MUUNGANO ndiyo sherehe za kuzaliwa TANZANIA sasa Tanzania bara imezaliwa lini?

    ReplyDelete
  5. Hakuna nchi inayoitwa Tanzania bara duniani iliyopsts uhuru decrmber 9,1961ni upotoshaji mkubwa wa historia, hivi kwa nini watawala wanaona aibu kusema TANGANYIKA? Utumwa wa kifikra

    ReplyDelete
  6. Uhuru wa Dec. 9,ni wa Tanganyika,mwaka 1961.Tanganyika iliungana na Zanzibar April 1964 ikazaa Tanzania. Mazoea yametufanya kutofautisha hii Tanzania yetu kama Tanzania bara na Visiwani(Zanzibar)ili kuipa heshima ya jina Tanzania. Kuna mambo yanayoeleweka internal si lazima ujulikane kimataifa kama wengine watakavyo. Kila pande ina historia yake tofauti katka harakati za uhuru wake. Hivyo,kila upande ni vizuri kusherehekea siku zake na ile ya umoja!!!Si vibaya. Kila kitu si lazima kijulikane kwa wazungu ili kiwe sahihi. Emancipate urself from mental slavery!!Nyerere gave u the political freedom. Now it's time for Africans to free ourselves from mentality za kitumwa!!Nawasilisha!!

    ReplyDelete
  7. wewe hapo juu ebu nifunze na zanzibar ilifutwa mwaka gani?

    ReplyDelete
  8. Yaani ss watanzania kweli bongolala...ingekujaje tanzania bara bila kua na muungano na zenji...neno tanzania limetokana na tanganyika na zanzibar..sasa how come mseme uhuru wa tz bara huo n upotoshaji wa hali ya juu

    ReplyDelete
  9. labda nitumie huu mfano.. BAADA YA MTU KUZAKIWA ANAWEZA KUITWA MWASINDI, NA AKABATIIZA UPYA KWA JINA LA FREDY, SOO TUNAPOFANYA BITHDAY ITAKUWA INAMHUSSU FREDY SIO MWASINDI, HIVYO TUTAITA NI SIKU YA KUZALIOWA FREDY,,,,,,,,,,,,

    ReplyDelete
  10. Wadau hapo juu uhuru wa Tanganyika utabaki kama ulivyo kihistoria (siyo wa Tanzania Bara)

    Na wewe mdau wa pili uliyeuliza kuhusu uhuru wa Zanzibar, huo ulipatikana December 10, 1963 kwani Tanganyika na Zanzibar zilikuwa nchi tofauti mpaka mwaka 1964 April.

    Naona wewe ndiyo huelewi historia ya nchi hii, hebu katafute reference books ambazo ni original na siyo zilizochakachuliwa.

    ReplyDelete
  11. Rais Mtarajiwa pendeza saaana wewe

    ReplyDelete
  12. Huu ni uninga. Jeshi la Muungano...bado unaulizia Tanganyika. Uhuru ni wa watu si wa jina la Tanganyika. Useme Tanzania au Tanganyika watu ni wale wale...shida iko wapi. idiot.

    ReplyDelete
  13. Tanganyika ipo ujerumani, hapa tunayo tanzania bara na visiwani, fulu stopu. Wewe mzanzibari kama hutaki kuitwa mtanzania visiwani basi hama katafute nchi nyingine au rudi kwenu uarabuni na bunjabi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...