Maalim Hassan Yahya Hussein amerudi rasmi kundini CCM baada ya kuwa nje ya chama kwa takriban miaka 20 hivi na ushee.
Maalim Hassan alijitosa katika safari yake ya kisiasa kwa kujiunga na CHADEMA ambapo katika  kipindi hicho aliwahi kugombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya chama hicho na pia udiwani kwa kupitia chama hicho hicho - lakini mara zote kura hazikutosha.
Juzi alipokekelewa kwa shangwe na wanachama wa CCM  katika kata ya Mzimuni, Magomeni, katika mkutano wa kuwanadi wagombea wa serikali za mitaa wakiongozwa na mwenyekiti wa kata ya Magomeni Ndg.  Hassan Dalali na diwani wa kata hiyo Ndg.  Chambuso.
Katika hotuba yake ya shukrani Maalim Hassan amewahakikishia  wanachama wa CCM kwamba atatumia uzoefu wake aliopata kwa wapinzani kukiimarisha chama kuelekea ushindi katika serikali za mitaa, udiwani,  ubunge na hadi urais.
"Upinzani hakuna dili na habari ya sasa ni CCM asikwambie mtu", Maalim Hassan aliiambia Globu ya Jamii, baada ya kukaribishwa tena kule alikokuita kundini baada ya kupotea maboya.
Maalim Hassan Yahaya Hussein akimwaga sera katika mkutano wa kumkaribisha kundini uliofanyika katika viwanja vya Mtambani Magomeni jijini Dar es salaam. Kulia ni mwenyekiti wa kata ya Magomeni Ndg. Hassan Dalali
Maalim Hassan Yahya Hussein akilakiwa kwa furaha baada ya kurudi kundini CCM
Maalim Hassan yahya Hussein akiwa katika  mkutano wa kuwanadi wagombea wa CCM  mtaa wa Mwinyimkuu.
Picha na Sultani Kipingo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Huyu mheshimiwa anasema upinzani hakuna dili. Papo hapo, aligombea vyeo huko huko upinzani, akakosa. Je, anaweza kutufafanulia anamaanisha nini anaposema huko hakuna dili, na kwa nini aligombea?

    Ninahisi kwamba alipokuwa huku CHADEMA, alisema CCM hakuna dili. Sitashangaa iwapo kesho na keshokutwa, atatimkia kwingine na kudai kuwa CCM hakuna dili. Yangu macho.

    ReplyDelete
  2. Prof. Mbele huyu Mhe. anatafuta 'dili' na sio uongozi kuwatumikia wananchi. Hata CCM atakosa hiyo 'dili' kwani watu wanataka kiongozi na sio mtafuta
    'dili'

    ReplyDelete
  3. Ni tamaa ya madaraka ndiyo imempeleka ccm na huko akikosa anachotaka pia ataondoka

    ReplyDelete
  4. Huyu naona anataka kujiaribia kazi yake ya unajimu/utabiri,siasa ni mchezo mchafu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...