Luiza Nyoni-Mbutu akipozi na mumewe Farijala Mbutu ambaye ni mtoto wa mwanamuziki wa zamani wa Orchestra Makassy Marehemu Mzee Simaro Aimala Mbutu. Farijala pia ni mwanamuziki hodari akiwa na Kilimanjaro Connection ambayo inapiga muziki ndani na nje ya nchi.
KIONGOZI wa bendi mpya ya Utalii Jazz Band ambaye pia mwanamuziki Mkongwe wa muziki wa dansi nchini ‘Komandoo Hamza kalala ama unaweza kumwita Mzee wa Madongo’ amethibitisha kushiriki katika onesho maalum la miaka 16 ya mwanamuziki Luizer Mbutu kuwa Twanga Pepeta.
Mkurugenzi wa Kampuni ya The African Stars Entertainment (ASET) Asha Baraka amesema kwamba Komandoo tayari amethibitisha kushiriki na hivyo usiku huo utakaofanyika Desemba 20 ndani ya ukumbi wa Mango Garden utakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wakongwe.
Pia alimtaja Stara Thomas ‘Stara T’ , Siza Mazongera 'Mamaa wa Segere’, pia wanafanya mazungumzo na wasanii mbalimbali ambao waliwahi kufanya kazi na Mbutu tangu bendi hiyo ilipoanzishwa kama vile Bob Gaddy, Banza Stone, Adolph Mbinga na wengineo.
Asha Baraka amesema kuwa wameandaa onyesho hilo ambalo litakua maalum kwa Kiongozi wa bendi hiyo ambaye anaetimiza miaka 16 ndani ya bendi bila kuhama tangu ilipoanzishwa.
“Uongozi wa ASET umeamua kuandaa usiku maalum wa kumuenzi Luiza kutokana na kua na msimamamo wa kukaa katika bendi kwa muda wote huo bila kuhama hilo ni jambo la kujivunia” alisema Asha.
Aliongeza kwa kusema kuwa onyesho hilo litakwenda kwa jina la Luiza Mbutu na Twanga Pepeta ambalo pia kutakuwa na shamrashamra zake ambazo zitatajwa siku itakapowadia” alisema Asha.
Pia aliongeza kwa kusema kuwa wao kama ASET wanatambua mchango wa Luiza ndani ya bendi hiyo hivyo kutakuwa na tukio laaina yake ambalo mashabiki na wadau wa bendi hiyo pamoja na wapenzi wa Luiza wajitokeze kwa wingi siku hiyo kushuhudia litakalojiri sambamba na kupata burudani kutoka kwa bendi ya Twanga Pepeta.Kiingilio kitakuwa sh. 10,000.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...