Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dr. Ali Mohammed Shein akikabidhi tuzo ya heshima ya mwanamichezo bora wa mwaka kwa Mama Fatma Karume Mjane wa Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyotolewa na Chama cha Waandishi wa habari za Michezo TASWA kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Usiku huu. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo TASWA Bw. Juma Pinto.)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dr. Ali Mohammed Shein akisoma hotuba yake mara baada ya kukabidhi tuzo hiyo kwa Mama Fatma Karume Mjane wa Marehemu Mzee Abeid Amani Karume kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam usiku huu.
Mama Fatma Karume akitoa nasaha zake kwa wanamichezo usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo TASWA Bw. Juma Pinto na Maulid Baraka wa Kitenge Mtangazaji wa Redio ya EFM ambaye alikuwa MC wa hafla hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...