Mahafali ya nane ya Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT), yanatarajiwa kufanyika
Januari 31 mwaka huu katika viwanja vya chuo hicho na yatatanguliwa na utoaji wa tuzo na
zawadi mbalimbali kwa wahitimu ambao wamefanya vizuri katika masomo yao.
Taarifa ya DIT kwa vyombo vya habari imesema kuwa tuzo kwa wanafunzi zitatolewa
Januari 23 mwaka huu ikiwa ni wiki moja kabla ya mahafali hayo ambayo wahitimu katika
ngazi na masomo tofauti watatunukiwa.
Wahitimu watakaotunukiwa ni siku hiyo ni pamoja na wa Stashahada ya Uhandisi
(Ordinary Diploma), cheti cha awali cha TEHAMA (IT) mwaka wa masomo
2013/2014.
Wahitimu wametakiwa kusoma utaratibu wa kuthibitisha kushiriki mahafali
hayo katika tovuti ya Taasisi www.dit.ac.tz na “Rehearsal” itafanyika Ijumaa
tarehe 30 Januari 2015.
“Malipo ya Tshs 30,000/= kwa ajili usajili yatafanyika kwenye tawi lolote la
NBC kwenye akaunti namba 018101003145 na kujisajili kupitia tovuti ya
Taasisi www.ac.dit.tz” Inasema taarifa hiyo.
Malipo yanatakiwa klufanyika kwa kutumia jina kamili kama linavyoonekana
kwenye orodha ya wahitimu iliyotolewa kwenye tovuti ya Taasisi, namba ya
usajili na dhumuni la malipo mf.
Ada, transcript na graduation.
Kulingana na taarifa hiyo, mwisho wa kujisajili ni tarehe 31 Desemba, 2014 na
wahitimu wametakiwa kufahamisha kuhusiana na mahafali hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...