Kundi zima la Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi, litafanya
utambulisho wa wimbo wao mpya “Sura Surambi” kwa wakazi wa
Morogogo Disemba 25 kwenye maadhimisho ya siku ya Christmas.
Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Ramadhani maarufu kama
Isha Mashauzi (pichani juu), ameuambia mtandao huu kuwa onyesho
hilo litafanyika ndani ya ukumbi wa Savoy Hotel na watasindikizwa
na mfalme wa kigodoro Msaga sumu.
Isha amesema “Sura Surambi” ni ngoma yao mpya kabisa iliyoachiwa
mwishoni mwa mwezi uliopita na Morogoro unakuwa ndio mji wa
kwanza baada ya Dar es Salaam, kuonjeshwa ladha ya wimbo huo
ambao unafanya vizuri sana kwenye vituo vya radio.
“Huu ni utunzi na uimbaji wangu mimi mwenyewe, sina mengi ya
kuongea zaidi ya kuwaahidi wakazi wa Morogoro burudani
iliyokwenda shule,” alisema Isha.
Sura Surambi ni maandalizi ya albam mpya ijayo ya Mashauzi Classic
ambapo tayari nyimbo mbili zimesharekodiwa, hii ikiwa ni pamoja na
“Ubaya Haulipizwi” ulioimbwa na Asia Mzinga, binti wa waimbaji
wakongwe wa taarab Abbas Mzinga na Bi Mwanamtama Amir.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...