
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliposimama kwenye Kijiji cha Ngeresero kwa ajili ya kuwaungisha wanawake wa kimasai wanaofanya biashara ya kuuza bidhaa mbalimbali za shanga kwa watalii wanaosimama kwenye kijiji hicho kwa ajili ya kupata mahitaji mbalimbali, wakati akielekea kijiji cha Ololosokwan kilichopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika lake la UNESCO.
Na Mwandishi wetu, Arusha
NDOTO ya kuwa na kijiji cha dijitali nchini Tanzania itaanza kutimia Januari mwakani wakati vifaa vinavyotakiwa kukamilisha mradi huo vitakapowasili kutoka kampuni ya Samsung Electronics.
Kwa mujibu wa watekelezaji wa mradi huo mkubwa unaotarajiwa kutumia dola za Marekani milioni 1, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) vifaa hivyo vinatarajiwa kuingia Bandari ya Dar es Salaam Januari tano mwakani.
Mkataba wa kuanzishwa kwa kijiji cha dijitali eneo la Ololosokwan tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro ulitiwa saini kati ya Unesco na Samsung electronics Novemba 6 mwaka huu.
Akizungumza na halmashauri ya kijiji cha Ololosokwan , Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues amewataka wanakijiji kujiandaa kwa mabadiliko makubwa ya kijiji chao kinapoingia katika dunia ya dijitali.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiwaonyesha jambo wakina mama wa kimasai jinsi gani teknolojia inayvowaleta watu kwa ukaribu zaidi kupitia "Tablet" ambapo katika kijiji hicho cha digitali cha Samsung wakazi wa eneo hilo watakua wakipewa mafunzo kutumia kifaa hicho cha "Tablet".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...