Maafisa
wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa Marehemu Capt.
Kidai Senzala Kalise aliyefariki Novemba 29 mwaka huu katika ajali ya
Helkopta iliyotokea Kipunguni B-Moshi Bar Dar es Salaam wakielekea
katika makaburi ya familia huko Gonja Maore Wilaya ya Same mkoa wa
Kilimanjaro Desemba 1, 2014.
Marehemu
Kidai alikuwa Mrakibu wa Polisi na alizikwa kwa heshima zote za
Kipolisi ikiwa ni kupigiwa mizinga na saluti mbalimbali za kipolisi
kabla na baada ya maziko yake.
Helkopta aina ya Robertson R44 iliyo tolewa msaada
kutoka kwa Taasisi ya Howard G.
Foundation inayomilikiwa na mfanyabiashara mashuhuri nchini Marekani Bw.
Warren
Buffet ililetwa nchini kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya ujangili
na kupokelewa nchini na Waziri wa Maliasili na Utalii June 14,
2014 jijini Dar es Salaam na kuikabidhi kwa Mamlaka ya Hifadhi za
Taifa Tanzania (TANAPA) ilipata ajali majira ya saa nne asubuhi baada
ya upata hitilafu katika injini yake na kupoteza maisha ya Mrakibu wa
Polisi Capt. Kidai Senzala Kaluse, Mkaguzi wa Polisi Capt. Simba Musa
Simba, Konstebo wa Polisi, Josso Selestine na Capt. Joseph Khalfan wa
Malisasili aliyezikwa Arusha.SOURCE: Father Kidevu Blog
Maofisa wa Polisi wakijiandaa kulibeba jeneza la Marehemu Capt Kidai.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...