Na
Bakari Issa,Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa
Mboni Show,Mboni Masimba ameamua
kuhamishia kipindi cha Mboni show
katika kituo cha utangazaji cha
Taifa (TBC) kutoka EATV ili kuvutia
watazamaji wengi na wapya kwa wazee
pamoja na vijana.
Kipindi cha
Mboni Show kitaanza kurushwa TBC kuanzia
January 2 mwaka 2015 siku ya
Ijumaa saa 3 Usiku-4Usiku na marudio
Jumanne saa 9:00
mchana-10:00mchana.
Akizungumza na
waandishi wa habari,mapema leo jijini Dar ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO),Mboni Masimba ametoa shukrani
kwa EATV kwa ushirikiano wao kwa
kipindi chote alichokuwa nao,na kusema
kuwa amehamishia kipindi cha Mboni Show katika kituo cha TBC ili kuvutia
watazamaji wengi hakuna atakaye tumia jina la Mboni Show
na hakuna kitakachomkwamisha kwa
vile ana hati miliki.
“Nimeamia TBC kwa kuwa nahitaji watazamaji wengi ,wote wazee na vijana na hakuna atakaye tumia jina langu la
Mboni Show kwa kuwa nina hati miliki ya
jina hili”alisema Mboni.
Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC,Bw.Fadhili Chilumba amesema wamefurahi kuwepo kwa Mboni Show katika kituo cha Taifa(TBC) na kutoa
wito kwa mashabiki kuweza kuwadhamini watu kama wakina Mboni na wanamkaribisha sana.
Nao wadhamini wa
Mboni Show,Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) wamesema
wanamwezesha Mboni kuwepo
hewani ili kuhamasisha,kuelimisha pamoja na kuburudisha umma wa Watanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...