Na Bakari  Issa,Dar  es Salaam.

Uongozi  wa  Tanzania Fellowship  Churches  unatarajia kufanya mkesha  mkubwa  kitaifa wa kuliombea  Taifa,Desemba 31 katika uwanja wa Taifa jijini  Dar es Salaam.

Mkesha huo una lengo la kuliweka Taifa mbele ya usalama wa Mungu pamoja na kupatikana amani  na utulivu kwa Taifa zima kwa ujumla.

Akithibitisha kuwepo kwa  mkesha huo   kitaifa,Mwenyekiti  wa mkesha  huo kitaifa,Mchungaji  Geodfrey  Mallasy  amesema mkesha huo una lengo  la kuliombea  Taifa  na kupatikana amani na utulivu.

“Mkesha huu una lengo la kuliweka Taifa  letu mbele ya usalama wa  Mungu na kuliombea Taifa letu  amani  na utulivu kutokana na bila amani hakuna kinachowezekana”alisema  Mallasy.

Aidha,Mallasy ameeleza kuwa mkesha huo  utahudhuliwa na mgeni rasmi ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Mohammed  Gharib Bilal badala ya Rais Jakaya Kikwete kuomba radhi kutokana na tatizo la kiafya.


Hata hivyo,uongozi  wa Tanzania Fellowship umeandaa usafiri kwa kampuni ya mabasi ya UDA kutoa huduma ya usafiri siku ya mkesha,pamoja na kutengeneza  timu moja ya waimbaji,kukusanya sadaka zikazosaidia kuandaa  mkesha mwingine utakaokuja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nchi yetu inahitaji maombi

    ReplyDelete
  2. Nadhani nia ingekua kuliombea Taifa tusipate njaa, tuwe na mvua za kutosha, maradhi yaondoke,watanzania wasome kwa bidii katiba pendekezwa mambo mengine yatapatikana kwa box la kura tu hayaombwi ktk viwanja......

    ReplyDelete
  3. Kuwakumbusha watu wafate kanuni za maadili na serikali pia.
    1. wasile rushwa
    2. serikali ilipe mshahra wa kikidhi ugumu wa maisha
    3. wasipendelee kwa misingi ya (kabila, dini, rangi, mahali, nk.
    4...

    tulishabarikiwa saana.

    sisi wajibu wetu ni kufuata maadili kwani tunataka Mungu ndo atufanye wanamaadili? Ye atasema ametupa utashi (free will) ili tuchague baraka au adhabu kwa kuchagua kitendo muafaka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...