Mhariri Msanifu wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya ametunukiwa Shahada ya Sayansi ya Jamii katika Siasa, Uongozi na Utawala (Political Scince and Public Administration), baada ya kuhitimu masomo yake ya elimu ya juu.

Mkotya pamoja na wahitimu wengine walitunukiwa shahada zao mwishoni mwa wiki wakati wa mahafali ya 26 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika eneo la Bungo, Kibaha mkoani Pwani.

Wahitimu wote walitunukiwa shahada zao na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dk. Asha Rose Migiro, ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria.

Katika mahafali hayo, mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd. Wengine ni Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Tolly Mbwette na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho Profesa Samuel Wangwe.
Mhariri Msanifu wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya (kati) akiwa na wahitumu wenzake wakipia kitabu cha ratiba ya mahafali yao hayo.
Pongezi kutoka kwa ndugu waliofika kwenye mahafali hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...