MDAU NGULI WA GLOBU YA JAMII MHANDISI MKWAWA AKA CHIEF AMELAMBA NONDOZZZ YA SHAHADA YA UZAMILI KTK UONGOZI WA BIASHARA-MBA (FINANCE) KUTOKA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA. HII NI SHAHADA YA PILI YA UZAMILI KUTUNUKIWA MWAKA HUU WA 2014, BAADA YA ILE YA MASTER OF ENGINEERING SCIENCE (METALLURGY) KUTOKA CHUO KIKUU CHA CURTIN (WASM) NCHINI AUSTRALIA MWEZI AUGUST 2014.
Mhandisi Mkwawa akivalishwa shada la maua na mai waifu  wake mamaa Warda muda mfupi baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara katika viwanja vya chuo kikuu huria huko  Bungo Kibaha.
Mhandisi Mkwawa akipongezwa  na Dada yake Bi Asha aka Mama Zeana kwa kazi nzuri ya kufanikiwa kutunukiwa shahada ya uzamili ktk uongozi na Biashara.
Chief Mkwawa  akila poooz na kukabidhiwa shada la Maua na shemeji yake Grace Njawa aka Mama mdogo huko Bungo Mkoani Pwani wakati wa Mahafali ya ishirini na sita ya chuo kikuu huria cha Tanzania.
Chief Mkwawa akipozi na Mai waifu wake pamoja na Chief Jr.muda mfupi baada ya kulamba Nondoooz .Hii ni shahada yake ya pili ya Uzamili kwa Mwaka 2014 baada ya ile ya  Master of Engineering Science in Metallurgy aliyotunukiwa nchini Australia mwezi August 2014.
 Mhandisi Mkwawa akila pooooz  na wahandisi wenzake ,Kutoka kushoto ni Mhandisi Mwandamizi Hassan Mogaeka kutoka nchini Australia akifuatiwa na Mhandisi Boniface Benedict Kyaruzi Kutoka NEMC na kulia kwa Chief ni Mhandsi Abdulrahman Milandu wa Wakala wa Ukaguzi Madini Tanzania (TMAA)  muda mfupi baada ya Chief Mkwawa kulamba Nondoooz .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. kwa lugha fasaha siku hizi inaitwa shahada ya umahiri sio ya uzamili

    ReplyDelete
  2. Nampongeza engineer wangu.Kila la heri mkuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...