Mdau Ramadhan Hussein ambaye ni Meneja wa Kiota maarufu jijini Mwanza "Villa Park",mwishoni mwa wiki iliyopia aliamua kuachana kabisa na Chama cha Makapera kwa kufunga pingu za maisha na Bi. Husna Salum mkazi wa huko Ukonga jijini Dar es Salaam.Ndoa yao hiyo ilifungwa katika Msikiti Mkubwa wa Ijumaa ulipo Airport,Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mdau Ramadhan Hussein na Mamsapu wake Bi. Husna Salum wakionekana kuwa na nyuso za furaha mara baada ya kumeremeta kwao.
Ni chereko chereko tu kwa kwenda mbele.
Maharusi wakipokea nasaha kidogo kutika kwa Wazee (hawapo pichani).
Wakiondoka nyumbani kwa Bi. Harusi.
Pongezi kutoka kwa Imamu wa Msikiti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...