Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa katika kikao na watendaji wa
kampuni ya DermCappello yenye Ubia kati ya Watanzania na Waitalia waliofika katika Ofisi za Wizara ya
Nishati na Madini ili kueleza nia yao ya kuzalisha umeme wa jua na kujenga kiwanda cha kutengeneza
vifaa vya umeme jua. Kutoka kushoto ni watendaji wa kampuni ya DermCapello, Eng. Steven Chaula,
Capello Giuseppe na Giuseppe Capello. Kulia ni Mchumi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Nicolaus
Moshi, Mwanasheria wa Wizara, Abbas Kisuju, na Eng. Innocent Luoga, kamishna Msaidizi Nishati
anayeshughulikia Umeme.
Rais wa kampuni ya Capello ya Italia, Capello Giuseppe akizungumza wakati wakati wa kikao kati ya kampuni hiyo na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini. Kampuni hiyo iliyoungana na watanzania na kuunda kampuni ya DermCapello walifika Wizara ya Nishati na Madini ili kueleza nia yao kuwekeza katika umeme wa jua.
Muwongo yupo kwa sana waliopiga kelele bungeni nadhani hawamfahamu JK subiri uone
ReplyDelete