Na Amina Hezron, Iringa.

Vijiji 31 vilivyopo mufundi kaskazini mkoani Iringa vinatarajia kupokea umeme na tayari baadhi ya vijiji vipo katika hatua ya mwisho ya kufunga vikombe kwaajili ya kuanza kuvuta nyaya.

Akizungumza na mwandishi wetu katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini ambae pia ni naibu waziri wa maliasili na utalii Babtist Mdende amesema kuwa, vijiji vinavyotarajia kupata umeme safari hii ni vile vijiji vilivyopo  tarafa ya sadani,ifwagi na kibengu.

“vijiji hivyo ni mapogoro, igomaa,kibada,ndolezi na vengine kama ugesa,vikula,ilasa na kipanga ambavyo upimaji bado unaendelea kwaajili ya kusimika nguzo, 

“kunabaadhi ya vijiji vipo katika hatua ya awali ya kusimamisha nguzo ikiwepo kijiji cha Isalavanu ambacho mradi wake wa umeme unashughulikiwa na TANESCO wilaya ya mufindi”, alisema Mdende.

Aidha Mdende ameeleza kuwa kwa wale watakao ingazwa kwa mara ya kwanza yaani watu wa kwanza wakati wa kuzindua mladi wa umeme wataingiziwa kwa gharama ya shilingi elfu 30.
Mbunge wa jimbo la mufindi wa kasikazini ambaye pia naibu waziri wa maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa  
Mbunge wa jimbo la mufindi wa kasikazini ambaye pia naibu waziri wa maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa akiwa na mkuu wa wilaya wa mufindi.
Mbunge wa jimbo la mufindi wa kasikazini ambaye pia naibu waziri wa maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa akiwa amevalia .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...