
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amelaumu watu fulani ndani ya chama tawala cha ZANU-PF kwamba wanapanga kumng'atua mamlakani.
Akihutubia
kongamano la chama hicho, Mugabe amesema kuwa kuna majaribio ya
kuwahonga wajumbe kumpinga kama kiongozi, lakini wajumbe hawawezi
kupokea hongo.
Kwa hilo amesema kuwa atapambana na rushwa ndani ya chama na kukabiliana na maafisa wa chama ambao kazi yao ni kutoa hongo.
Wanachama wengi wa chama hicho wangali ni wafuasi sugu wa Rais Mugabe

Hasira ya Mugabe iliokana na madai ya njama ya kumuua yaliyotolewa
dhidi ya naibu wake Joyce Mujuru. Hata hivyo Mujuru alikanusha madai
hayo ambayo yamekuwa yakimuandamana.
Mugabe alisema kutokuwepo kwa Bi Mujuru kwenye mkutano huo wa chama kunaonyesha kuwa anaogopa.
Kadhalika Mugabe amesema Mujuru ni mwizi anayepanga kumuondoa mamlakani kwa kushirikiana na maafisa wengine wa chama.
Maelfu ya wajumbe wa chama walihudhuria kongamano hilo mjini Harare

Chama tawala cha Zimbabwe kinakumbwa na vita vya ndani kwa ndani
kuhusu ni nani atakayerithi nafasi ya Mugabe ambaye ana miaka 91 na
ameilongoza taifa hilo tangu lijinyakulie uhuru.
Vilveile kiongozi huyo ametupilia mbali dhana ya kujiuzulu akisema ni upuzi .
Hivi karibuni afisa mwingine mkuu wa chama tawala, Robert Gumbo aliambia
BBC kwamba Mugabe amwenye umri wa miaka 90 amegeuza chama tawala na
kukifanya mali yake binafsi.

Bi Joyce Mujuru amedaiwa kupanga njama ya kumuua Mugabe ili achukue mamlaka kutokla kwake.
Bwana Gumbo alisema kuwa lengo kuu la Mugabe ilikuwa kuendeleza uongozi wa chama kwa niaba ya mke wake Grace.
Bi
Mujuru ambaye amekanusha madai hayo alionekana kama mtu ambaye
anegchukua uskani wa chama kutoka kwa Mugabe ambaye walipigania naye
uhuru wa nchi hio kutoka mikononi mwa watwala wazungu.
CHANZO: BBC SWAHILI
Ningekutana na Mugabe ningemwambia amuachie mama Joyce yeye abaki kiongozi wa chama
ReplyDeleteUzushi wa viongozi wengi wa Afrika ni kung'ang'ania madarka na hakuna mapinduzi wanayofanya zaidi ya kuwaletea umaskini watu na wao kunufaika zaidi. Miaka 91 bado sing'atuki ng'o in maana gani" huo ni ulafi wa madaraka. Badilikeni
ReplyDeleteMugabe na marehemu banda wa Malawi hawana tofauti anataka afie madarakani wamuache tu kwa sasa kwanza hatawali kutwa analala tu baba wa watu.
ReplyDeletemdau.
mozambique