Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Joseph ole Lenku (kulia), na Mkuu wa Polisi, David Kimaiyo ambae  amejiuzulu  muda mfupi leo 

Kufuatia  shambulio  lililofanywa na  kundi la wanamgambo wa Al Shabaad  nchini Kenya kwa  kuwaua   watu  36 yaliyotokea  leo  ,mkuu wa polisi  nchini humu  David Kimaiyo anadaiwa  kutangaza  kujiuzulu nafasi  yake  hiyo.

Mkuu   huyo wa  polisi amelazimika  kujiwajibisha  mwenyewe kwa  kujiuzulu  kutokana na mauwaji ya mara kwa mara  yanayofanywa na kundi  hilo la Al shabaad nchini  humo kwa  kipindi  cha siku takribani 8  ni  watu zaidi ya 60  wameuwawa  na kundi hilo wakiwemo  wale  waliotekwa katika basi na kumiminiwa  risasi na Al Shabaab .

Suala  hili  la kujiwajibisha  kwa  wenzetu  Kenya  wanaweza  hasa  wakitambua kuwa  cheo ni  dhamana  ila ingekuwa  kwetu Tanzania kwa  kiongozi  kujiuzulu bila  kuundiwa  tume ni  vigumu  sana   

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. uWAJIBIKAJI, PIA KUNA WAZIRI KAPIGWA CHINI NA UHURU HAYO NDIO MAMBO SIO BLAH BLAH....HATUFIKI WATU WANAJIFANYIA WATAKAVYO....

    ReplyDelete
  2. Uwajibikaji ni muhimu, lakini vita hii na Alshabab Mungu asaidie iishe wakenya wakae kwa amani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...