Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kisumba, Jimbo la Kalambo, mkoani Rukwa, katika mfululizo wa mikutano ya ziara ya Operesheni Delete CCM katika vijiji vya mkoa huo
 Naibu akikumbatiana na mzee ambaye alikuwa mmoja wa wasikilizaji kwenye mkutano wa Operesheni Delete CCM uliofanyika katika Kijiji cha Samazi, mkoani Rukwa. Mzee huyo ambaye alitokwa na machozi wakati akisikiliza hotuba, alisema kuwa aliguswa sana na maneno ya Mwalimu.
 Naibu Katibu Mkuu akiagana na wananchi wa kijiji cha Kisumba baada ya mkutano huo wa hadhara kijijini hapo.
Naibu Katibu mkuu na msafara wake wakishiriki chakula walichoandaliwa na wenyeji wao katika Kijiji cha Samazi Jimbo la Kalambo, baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo ikiwa ni mwendelezo wa mikutano mfululizo wa Operesheni Delete CCM mkoani Rukwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Inasikitisha ukiona hali za watu wa vijijini na jinsi Mapesa ya serikali yanavyotafunya na wachache wakishirikiana na watu ambao hawana hata asili ya Tanzania.

    ReplyDelete
  2. Mwalimu umetema madolali ya Voda sasa umejikita huku? Au unaangalia ubunge 2015 kwani ni ulaji zaidi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...