Ruth Bura, Mratibu wa Bima ya Elimu Bayport Tanzania kulia akimkabidhi hundi bwana Kennedy Kaupenda kwa ajili ya kuendelea na masomo ya elimu ya juu baada ya kufariki mzazi wake.
Mratibu wa Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania, Ruth Bura kulia, akizungumza jambo katika makabidhiano ya hundi kwa bwana Kennedy Kaupenda kushoto kwake, Makao Makuu ya Bayport, mapema wiki hii.
TAASISI ya kifedha ya inayojihusisha na mambo ya mikopo ya Bayport Tanzania, imempatia Sh Milioni tatu (3,000,000) mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa (MUCE), Kennedy Kaupenda, kufuatia huduma mpya ya Bima ya Elimu inayoendeshwa na taasisi hiyo nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...