Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
Matukio ya kutishia amani ya nchi na usalama wa raia yatapungua kama mabalozi wa nyumba kumi watafanya kazi zao kwa uaminifu kwani wao ni viongozi wa kwanza walio karibu na wananchi hivyo basi wanatakiwa kuwafahamu wakazi wa maeneo yao.
Hayo yamesemwa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Vuai Ally Vuai wakati akifungua semina ya siku moja ya uwezeshaji wa chama hicho kwa mabalozi (viongozi wa mashina) wa wilaya ya Lindi mjini.
Vuai alisema Balozi ni kiongozi wa kwanza anayetakiwa kujua idadi ya wakazi wake, kazi wanazozifanya na majina yao kitendo ambacho kitasaidia kuimarisha usalama wa eneo husika lakini miaka ya hivi karibuni wameacha kufanya kazi hiyo kwa uadilifu na kuviachia vyombo vya dola pekee.
“Jukumu la kulinda amani ya nchi na usalama wa taifa letu ni la kila mtu, lakini hivi sasa kazi hiyo vimeachiwa vyombo vya dola pekee, mabalozi fanyeni kazi ya kuwatambua wakazi wa maeneo mnayoishi hii itasaidia kumtambua mualifu pale atakapofika katika eneo lenu”, alisema Vuai.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...