NAIBU
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuongoza Tamasha Maalumu
la 'Upendo wa Mama' linalotarajiwa kufanyika katika Kanisa la Rutheran
Mabibo Extenal jijini Dar es Salaam na kushirikisha waimbaji wengi
kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Akizungumzia
tamasha hilo leo jijini Dar es Salaam, Rais wa taasisi ya Upendo kwa
Mama Foundation yenye makao makuu yake mkoani Arusha, Injinia Carlos
Mkundi alisema Naibu Waziri Nchemba ndiye mgeni rasmi wa Tamasha hilo
maalumu ambalo pamoja na mambo mengine linafanyika kutambua mchango
mkubwa wa mama kuanzia katika ngazi ya familia na jamii nzima.
Injinia Mkundi alisema tamasha hilo litakalofanyika Januari Mosi, 2015
chini ya uratibu wa Taasisi ya Upendo kwa Mama Faundation,
litashirikisha waimbaji wa injili akiwemo Faraja Ntaboba kutoka Congo,
Stella Joel, Ado Novemba, Jane Misso, Edson Mwasabwite wote kutoka
jijini Dar es Salaam.
Na
Rose Molel, Helen Kigazi wote kutoka mkoani Arusha.
Injinia Carlos Mkundi na mwimbaji wa muziki wa injili ambaye naye
atatumbuiza katika tamasha hilo, aliwataja waimbaji wengine ambao
watashiriki katika tamasha ni pamoja na Mbunge, Matha Mlatta, Kwaya ya
Mamajusi kutoka Moshi, mwimbaji Tumaini Njole, Messi Chengula na
waimbaji wengine wengi.
"...Washiriki
kila mmoja anaweza kuja na mamayake anayempenda pamoja na zawadi yake
maalum, ambayo atamkabidhi wakati itakapotangazwa...kutakuwa na waimbaji
wa muziki wa injili kutoka nje na ndani ya nchi ili kuleta mvuto zaidi
tunawaomba wananchi wajitokeze zaidi kuja kutambua mchango wa mama na
kuonesha upendo kwa mama zao," alisema Injinia Mkundi.
Akifafanua
zaidi alisema Tamasha la Upendo kwa Mama litakuwa la bure na litaanza
majira ya saa saba mchana siku hiyo na kuendelea hadi jioni
litakapofungwa. Alisema siku hiyo washiriki wanaombwa kuja na zawadi
maalumu ambayo kila mmoja atamkabidhi mamayake anayempenda katika
familia zao.
Rais wa Taasisi ya Upendo kwa Mama Faundation, Injinia Caros aliongeza
kuwa lengo lingine ni pamoja na kuwatia moyo akinamama na kuwaonesha
upendo juu ya kazi kubwa wanayoifanya katika familia zao na jamii kwa
ujumla.
Alisema
baada ya uzinduzi wa tamasha hilo kanisani hapo yataandaliwa matamasha
mengine makubwa na kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa
pamoja na mengine katika mikoa mbalimbali. Aidha aliongeza tamasha kama
hilo pia lilifanyika mkoani Arusha Novemba 16, 2014 katika uwanja wa
Sheikh Amri Abeib na kuwashirikisha akinamama zaidi ya 40,000.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...