Na Mwandishi Wetu

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, Desemba 28, 2014 (kesho J’pili) atafanya mkutano mkubwa kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na wananchi wa Singida Vijijini na Watanzania wote kwa kutimiza miaka 15 ya ubunge.


Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Mbunge huyo, Elia Diga, imesema kuwa mkutano huo ambao utaambatana na burudani mbalimbali, utafanyika katika Kata ya Ilongero na utahudhuriwa na viongozi wa Chama na serikali, viongozi wa dini zote na wananchi zaidi ya 20,000 kutoka kata zote zinazounda jimbo hilo na zile za jirani.



Katika mkutano huo, Nyalandu atahutubia wananchi pamoja na kueleza mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi chote cha miaka 15.



Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana mpaka sasa, Nyalandu pia ataeleza wananchi mwelekeo mpya wa jimbo hilo na mahali anapopenda lifike.



Viongozi wote wa CCM Wilaya ya Singida wakiongozwa na mwenyekiti wake, watahudhuria mkutano huo na kutoa hotuba fupi kwa wananchi.



Wasanii nyota wanaotamba nchini wakiongozwa na kundi la Makomandoo, Rose Muhando, Christina Shusho, H-Baba, Mchekeshaji Steve Nyerere na Bendi ya New Life Bandi watakuwepo kukonga nyoyo.



Pia kutakuwepo na vikundi  mbalimbali vya ngoma za asili vikiwemo Njagmba, Ilongero Group na vingine vingi vitakuwepo kutoa burudani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...