Benki ya NMB jana ilizindua rasmi tawi Jipya katika wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro. Tawi hili
linakadiriwa kuhudumia Zaidi ya wateja Mia moja kwa siku.
Tawi jipya la NMB Siha litakuwa linatoa huduma zote za kibenki kunzia kufungua akaunti mbali
mbali za akiba, huduma za mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya mahitaji yote kwenye
soko, huduma za fedha za kigeni, kukusanya mapato na kulipa kwa niaba ya serikali na taasisi
mbalimbali, kuweka na kutoa fedha.
Tawi la NMB Siha lipo maeneo ya Boma Ng’ombe bara bara ya Sanya Juu.Tawi hili linatoa
huduma kwa wakazi wa Lawate, Ngare Nairobi, Kibong’oto,Sanya Juu na Halmashauri ya wilaya
ya Siha kwa ujumla.
Naibu Waziri wa nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Aggrey Mwanri akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Siha mkoani Kilimanjaro. Wa Pili kutoka kushoto ni Meneja
wa NMB Kanda ya kaskazini - Bi.Vicky Bishubo pamoja na maofisa wengine wa NMB na serikali
wakishuhudia.
Meneja waTawi la NMB Siha Bw.Jovin Twesige akimsubiri Naibu Waziri wa nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Aggrey Mwanri ambaye anaweka saini kwenye Kitabu cha wageni wakati alipowasili katika tawi la NMB Siha Kwa ajili ya uzinduzi rasmi
Tawi hilo lipo eneo la Sanya Juu na siyo Boma ng'ombe, Bomang'ombe ipo wilaya ya Hai na siyo Siha, kuweni waangalifu kabla ya kutoa habari
ReplyDelete