Benki ya NMB jana ilizindua rasmi tawi Jipya katika wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro. Tawi hili linakadiriwa kuhudumia Zaidi ya wateja Mia moja kwa siku. Tawi jipya la NMB Siha litakuwa linatoa huduma zote za kibenki kunzia kufungua akaunti mbali mbali za akiba, huduma za mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya mahitaji yote kwenye soko, huduma za fedha za kigeni, kukusanya mapato na kulipa kwa niaba ya serikali na taasisi mbalimbali, kuweka na kutoa fedha. 

 Tawi la NMB Siha lipo maeneo ya Boma Ng’ombe bara bara ya Sanya Juu.Tawi hili linatoa huduma kwa wakazi wa Lawate, Ngare Nairobi, Kibong’oto,Sanya Juu na Halmashauri ya wilaya ya Siha kwa ujumla.
Naibu Waziri wa nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.  Aggrey Mwanri   akikata utepe kuashiria  uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Siha mkoani Kilimanjaro.  Wa Pili kutoka kushoto  ni Meneja wa NMB Kanda ya kaskazini - Bi.Vicky Bishubo pamoja na maofisa wengine wa NMB na serikali wakishuhudia.
Meneja waTawi la NMB Siha Bw.Jovin Twesige akimsubiri Naibu Waziri wa nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.  Aggrey Mwanri  ambaye anaweka saini kwenye Kitabu cha wageni wakati   alipowasili katika tawi la NMB Siha Kwa ajili ya uzinduzi rasmi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tawi hilo lipo eneo la Sanya Juu na siyo Boma ng'ombe, Bomang'ombe ipo wilaya ya Hai na siyo Siha, kuweni waangalifu kabla ya kutoa habari

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...