theNkoromo Blog, Singida
Mbunge wa Singida Kaskazini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwakani.

Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona kwamba anao uwezo wa kuiongoza Tanzania, katika harakati za kuwafikisha kwenye maendeleo endelevu wanayotaka Watanzania.

Amesema, yuko tayari kushindanishwa na Watanzania wengine watakaoona kuwa wanafaa kuwa Rais, lakini akisema kwanza kila atakayejitokeza itabidi kazi zake zipimwe kwa moto na endapo zitayeyuka hafai.

Nyalandu ambaye alitangaza uamuzi huo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo jimbo la Singida Kaskazini, alisema, yeye anaingia kwenye kinyang'anyiro akiwa kifua mbele kutokana na kuamini kwamba amekwishafanyakazi zilizotukuka.

"Kazi zangu nilizofanya zinajulikana na ninaziamini kwamba ni nzuri, hivyo yeyote atakayetaka urais apimanishwe na mimi kwa kupimwa kazi zetu kwa moto", alisema Nyalandu

Itakapofika siku ya siku, nitaenda Dodoma nikisindikizwa na wana Singida Mashariki, na wengine wengi kutoka pembe zote za Tanzania, kwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM", alisema.

Mkutano huo wa jimbo ambao ulipambwa na shamrashamra mbalimbali zikiwemo za wasanii wakiwemo kina Rose Mhando, ulifurika maelfu ya wananchi waliohamasika kumsikiliza Nyalandu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hongera Nyalandu. Unaonyesha kujiamini kama mwanasiasa. Tunaomba wengi hasa vijana mjitokeze kugombea uraisi.

    ReplyDelete
  2. Hongera Nyalandu kwa ujasiri wa kujitangaza. Tutakupa support kwa asilimia 100.

    ReplyDelete
  3. No chance mate! michuzi weka hii.

    ReplyDelete
  4. kuna uwezekano wa kukosa kura hata kwenye jimbo lako, kura za Taifa utazipata wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...