
Puljim ambaye alichukua nafasi ya Ernie Brandts mwaka jana kabla ya kutimuliwa mara baada ya mechi ya Mtani Jembe mwaka jana ambapo Yanga ilinyukwa mabao 3-1 alimtumia Kaseja kuwa nahodha katika kikosi chake lakini leo amesema anasikia uchungu kumkosa mlinda mlango huyo.

![]() |
Kavumbagu |
Puljim alisema "Nawaheshimu wachezaji waliopo, nimeshaongea nao jana (Jumamosi) ikiwa ni mazoezi yangu ya kwanza kufanya nao. Kikubwa nimewambia wasahau yaliyopita, wasisikitike kuondoka kwa wenzao wasisikitike kuondoka kwa kocha. Yaliyopita yamepita sasa tuanze maisha mapya, tukiwa na lengo moja la kuifanya Yanga iwe juu.
"Kikubwa nilichowataka ni kujitambua, Yanga ni klabu kubwa. Kama mchezaji anapata nafasi basi lazima ajue jukumu lake. Mkakati wangu ni kuhakikisha Yanga inacheza soka la kuvutia na mpangilio mzuri. Najua wote ni binadamu na kuna makosa ya kibinadamu hutokea lakini ninawataka kila mmoja acheze kiushindani na morali ya hali ya juu.
"Kazi yangu kama kocha ni kuwajengea wachezaji morali, naipenda timu yangu, tunatakiwa tushirikiane viongozi watimize wajibu wao, mimi kama kocha nitimieze wajibu wangu, na wachezaji pia watimize wajibu wao wacheze kwa kutumia akili na soka la kuvutia.
![]() |
Kiiza |
Hata hivyo, Pluljim aligoma kuweka wazi fomesheni atakayotumia kuhakikisha Yanga inachukua taji la Ligi Kuu msimu huu kwa kile alichodai kuwa fomesheni sio inayofanya kushinda mchezo.
"Ushirikiano na kujituma ndio kunakowezesha kushinda mchezo, sina hofu na wachezaji, nina hofu na mbinu zangu nitakazowapa kama watazielewa na kuzitekeleza, kuna wachezaji wapya ambao siwafahamu miezi minne ya michache kusema naweza kuiweka Yanga kwenye kiwango cha juu, litawezekana kukiwa na ushirikiano wa kutosha."alisema
Puljim amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu wa kuionoa timu hiyo hata hivyo amedai kuwa Yanga ni nyumbani itakapotokea ametimuliwa kabla ya muda wake kumalizika basi ataheshimu maamuzi ya uongozi ingawa hategemei hilo kutokea, kwa kuwa yeye ni mwanachama wa Yanga na amerudi nyumbani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...