Mkandarasi
wa soko kuu la Mwanjelwa linaloendelea kujengwa jijini mbeya
ndugu,Balwinder Singh
kutoka katika kampuni ya (NECCO) amezungumza na Ripota wetu juu ya
maendeleo ya soko hilo kubwa lenye zaidi ya maduka 400 ya biashara
ndogondogo,Benki mbili na kituo kikubwa cha polisi ambapo amesema soko
hilo anatarajia kulikabidhii mwakani (2015) mwezi wa tano.
Akiendelea
kuzumza,Mkandarasi huyo amesema kuwa hali ya Ujenzi inaendelea vyema na
wapo kwenye hatua za mwisho,hivyo hadi mwezi Mei mwakani soko litakuwa
limekamirika kabisa na kulikabidhi.
Mkandarasi wa Ujenzi wa Soko kuu la Mwanjelwa jijini Mbeya,Balwinder Singh akiandika baadhi ya maelezo ya vipimo muhimu vya Ujenzi kama alivyokutwa na Kameramani wetu.
muonekano wa mbele wa soko la Mwanjelwa.
muonekano wa nyuma wa soko hilo.
Hongera sana Jiji la Mbeya! Maendeleo kama hayo ni hatua muhimu katika kukua kwa uchumi wa Jiji na wananchi kwa ujumla. Soko linaonyesha lina hadhi ya kimataifa, hivyo mjitahidi kufanya biashara kitaalam zaidi.
ReplyDelete