Rais Mstaafu wa awamu ya pili nchini Tanzania,Alhaj Ali Hassan Mwinyi ametembelea miradi mbalimbali ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambapo aliweza kutembelea na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni, daraja ambalo linategemea kukamilika mwezi wa saba mwaka 2015 na vilevile amepata nafasi ya kutembelea Ujenzi wa nyumba za shirika la NSSF ambao unaendelea katika eneo la Mtoni Kijichi Kigamboni na baadhi ya nyumba hizo zimeishauzwa. Pia Rais Mstaafu aliweza kutembelea ujenzi wa mji mpya wa Dege uliopo eneo la Kigamboni jijini Dar.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Injinia Abubakar Rajabu akifafanua jambo baada ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kufanya ziara ya kutembelea ujenzi wa Daraja la Kigamboni,Nyumba za Mtoni Kijichi na Ujenzi wa mji mpya wa Dege.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dk. Ramadhan Dau (wa kwanza kulia) akimweleza jambo Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi alipofanya ziara yake kuona ujenzi mkubwa unaodhaminiwa na NSSF.
BOFYA HAPA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA PICHA ZAIDI
Du dege village kuzuri sana lazima niamie huko
ReplyDelete