Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.
 Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akibadilishana hati ya  mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania waliosaini kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.
 Baadhi ya waandishi wa habari na watumishi wa wizara ya Fedha pamoja na wawakilishi wa Serikali ya Saudi Arabia wakiwashuhudia Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas wakisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.(Picha zote na Eleuteri Mangi- Maelezo)
 
Eleuteri Mangi- MAELEZO
04/12/2014
Serikali ya Tanzania imesainiana  mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa zaidi ya  shilingi bilioni 45.2 na Shirika la Maendeleo la Saudia kwa lengo la kuboresha miradi wa maji kwa wilaya ya Same, Mwanga na ujenzi na ukarabati wa barabara Visiwani Zanzibar.

Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.

Akiongea na waandishi wa habari katika hafla hiyo, Waziri Saada alisema kuwa kati ya mkopo huo shilingi bilioni 41.25 ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani milioni 25 zitagharimia mradi wa maji katika wilaya za Same na Mwanga na  shilingi bilioni 3.96 kwa ajili ya maradi wa barabara Pemba, visiwani Zanzibar.

Waziri Saada alilishukuru Shirika la Maendeleo la Saudia kwa jitihada zao za kuisaidia Serikali ya Tanzania katika kautatua tatizo la maji wilaya za Same na Mwanga pamoja na uboreshaji wa barabara katika visiwa vya Pemba.
 
Aidha, mradi wa maji wa Same- Mwanga utagharimu Dola za Kimarekani milioni 110.34 ambazo benki ya BADEA, Shirika la Maendeleo Kuweit, OPEC na mashirika mengine wamekubali kukamilisha sehemu ya fedha iliyobakia.

Mradi wa maji wa Same- Mwanga baada ya kukamilika utasaidia kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji vijijini amabapo utasaida kuboresha hali ya maisha wa wananchi wa maeneo hayo, upatikanaji nwa maji safi na salama kwa maendeleo ya afya za wakazi hao na kuboresha uchumi wao kwa kutumia muda mwingi kwa shuighuli za uzalishaji mali badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas amesema kuwa makataba waliosaini leo unaonesha kuwa Saudi Arabia iko mstari wa mbele katika kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi wake kwa kuzingatia mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa waandishi wa habari na baadhi ya watumishi wa wizara ya Fedha na wawakilishi wa Serikali ya Saudi Arabia.

Mwisho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mkwanja mwengine huuuooo wa kugawana

    ReplyDelete
  2. Wametafuta mwingine ili wagawane duh

    ReplyDelete
  3. Hao watagawana kabla ya New Year mkwanja huo

    ReplyDelete
  4. Yap kama kawaida bila aibu zitaliwa zote m

    ReplyDelete
  5. Haya mafisadi gawaneni sisi wananchi tutalipa musiwe na wasi mabosi wenu tupo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...