WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi wakati wa Tamasha la Krismas Desemba 25 mwaka huu Uwanja wa Sokoine,
Mbeya.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati
ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa maandalizi kuhusiana na
tamasha hilo yanaenda vizuri.
“Tulikubaliana katika kamati tumuombe Waziri Mkuu mstaafu Sumaye
aje atupe baraka kwenye tamasha la Krismasi, nafurahi kusema ni mtu wa watu,
amekubali kujumuika na wadau wengine siku hiyo. Hili ni jambo la furaha kubwa
kwetu.
“Wasanii mbalimbali tunaendelea kuzungumza nao kuhakikisha
wanashiriki katika tamasha hilo,” alisema Msama katika taarifa yake. Sumaye alikuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Tatu
kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005, akiwa ndiye Waziri Mkuu aliyekaa muda mrefu
katika wadhifa huo kwa historia ya Tanzania.
Alisema wamepanga kufanya maboresho makubwa katika tamasha hilo na
moja ya maboresho hayo ni kuweka kiingilio rahisi zaidi ili kila mmoja aweze
kuhudhuria na kupata baraka kutoka kwa waimbaji hao wanaomsifu Mungu. “Waimbaji wote maafuru wa muziki wa Injili watakuwepo, kwani
tumejipanga vizuri mno kuhakiksha kwamba tamasha hili litakuwa gumzo kila mahali.
“Wapendwa wajiandae kushiriki kwa wingi kwani watashiba kiroho
kutokana na kuwa na waimbaji wengi wenye hamasa ya kiroho,” anasema. Baada ya
onesho la Desemba 25 mkoani Mbeya, siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Samora
Iringa na Desemba 28 Uwanja wa Majimaji Songea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...