Wasanii wa Hip hop katika anga ya muziki wa Bongofleva,Faridi Kubanda a.k.a Fid Q pamoja na Stamina wakilishambulia jukwaa kwenye tamasha la wazi la Tuo8January,hapo jana katika viwanja vya sabasaba mjini Morogoro.

Tuo8January ni kampeni maalum iliyozinduliwa hivi karibuni ikiwa na lengo la kuwahamasisha vijana kujitokeza kushiriki mchakato wa uchaguzi  wa viongozi mbalimbali wanaowataka na wanaowaamini wana uwezo wa kuleta mabadiliko ya kinidhamu kwenye masuala ya msingi ya Taifa letu.

Kama vile haitoshi kampeni hiyo inatumika kuwahamasisha vijana wenye uwezo na sifa za kugombea nafasi za uongozi kuchukua hatua sasa za kufanya hivyo,pia kupata vijana wen,vijana wenye vigezo vya kupiga kura pia ni lazima wafanye hivyo maana ni wajibu wetu na kuwa vijana ni lazima tushiriki kikamilifu katika mchakato wa kampeni ili kuhakikisha mambo ya msingi yanajadiliwa na wagombea na yanapewa kipaumbele. 

Katika tamasha hilo Fid Q aliwahamasisha vijana mbalimbali waliojitokeza kwenye tamasha hilo,kuwa imefika wakati wa vijana kujitokeza kushiriki mambo mbalimbali ya kimsingi kwa manufaa ya nchi yao na si kukaa chini na kuanza kulalama,wakati kwenye mambo ya maamuzi wakishirikishwa hawataki kujitokeza,hivyo ni wakati wao wa kuamka na kuchagua kiongozi kijana wa kisasa na si kiongozi wa kisiasa.
 Msanii mwingine wa hip hop katika anga ya Bongofleva,ambaye amekuwa akifanya vyema kwenye muziki huo,Niki wa Pili akitumbuiza katika jukwaa la wazi la Tuo8Januari lililofanyika mjini Morogoro hapo jana.
 Baadhi ya wakazi wa mji wa Morogoro wakishangilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika jana kwenye viwanja vya sabasaba mjini humo,tamasha hilo la wazi ambalo limewashirikisha wasanii mbalimbali,ni kampeni maalum ya kuwahamasisha vijana kushiriki katika chaguzi mbalimbali kwa njia ya matamasha.

Kampeni hiyo ilizinduliwa jijini Dar hivi karibuni na kufanyika tamasha la kwanza mkoani Njombe na sasa Mkoani Morogoro.Baadhi ya Wasanii mbalimbali wenye ushawishi mkubwa kwa vijana wameonesha kuiunga mkono kampeni hiyo,akiwemo Babu Tale, Mwana FA, Nick wa Pili, Lamar, P-Funk, Mwasiti, Barnaba, Ditto,G-nako,Fid Q,Shilole,Yamoto Band,Stamina na wengineo.

 Baadhi ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika jukwaa la tamasha la Tuo8January,lililofanyika jana katika viwanja vya Sabasaba,mjini Morogoro.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...