Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula
mbalimbali kwa Bi. Honorata wa kituo cha kulelea watoto yatima cha
Honorata kilichopo Temeke jijini Dar es salaam leo wakati alipokabidhi
msaada wa vyakula kwa vituo mbalimbali vya jijini Dar es salaam ikiwa ni
zawadi yake ya sikukuu ya Krismas kwa vituo hivyo, Bw. Alex Msama
amesema pia katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika kesho wakati wa
sikukuu ya Krismas mkoani Mbeya, kiasi cha fedha zitakazopatikana
zitakwenda kulipia ada za watoto yatima katika vituo mbalimbali
vitakavyofikiwa na msaada huo, Ameongeza kwamba msaada huo wa vyakula
una thamani ya shilingi milioni Nne na Nusu. Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula
mbalimbali kwa Bi. Halima Mpeta wa kituo cha kulelea watoto yatima cha
Mwandaliwa kilichopo Mbweni jijini Dar es salaam. Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula
mbalimbali kwa Bw. Rashid Mpinda katibu wa kituo cha kulelea watoto
yatima cha Maunga Centre cha Kinondoni. Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akigwa vyakula mbalimbali
baada ya kukabidhi kwa vituo vya kulelea watoto yatima jijini Dar es
salaam. Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo kwa
wanahabari mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa vituo vya
kulelea watoto yatimajijini Dar es salaam.
Home
Unlabelled
ALEX MSAMA AMWAGA ZAWADI ZA KRISMAS KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...