Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeshirikiana na Timu ya mpira wa miguu ya Sunderland (SAFC) ya nchini Uingereza katika uzinduzi wa utangazaji utalii wa Tanzania pamoja na kuhamasisha uwekezaji kwenye sekta ya michezo (Destination Partner in Tourism and Sports Development). Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 29 Novemba, 2014 kwenye kiwanja kinachomilikiwa na timu ya Sunderland “Stadium of Light”
Kwenye tukio hilo ambalo lilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe pamoja na, maafisa kutoka Bodi ya Utalii, Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza pamoja na watanzania waishio nchini Uingereza. Tukio hili lilifanyika wakati timu ya Mpira ya Sunderland ilipoikaribisha timu ya mpira ya Chelasea Football club.
Wakati wa uzinduzi huo matangazo ya Utalii yaliweza kurushwa katika kingo za kuta za uwanja wa timu ya Sunderland na kuonesha vivutio vya vivutio vya utalii wa Tanzania na vile vile yalioneshwa kwenye luniga kubwa iliyokuwepo kwenye uwajani huo. Aidha wachezaji wa timu ya Sunderland walivaa jezi maalum zilizoandikwa ‘Visit Tanzania’ wakati wakifanya mazoezi mepesi kabla ya mechi kuanza.
Bodi ya Utalii Tanzania ilitumia fursa ya uziduzi huu kuhamasisha wataliii kutoka ndani na nje ya Uingereza pamoja na mashabiki wa timu hizo kutembelea vivutio vya utalii wa Tanzania.

Mtu mwenye seaason ticket holder sio wa kusafiri kwenda Tanzania,na watazamaji mpira sio wapenzi wa likizo fupi bali watu wa kipato cha juu ambao wanafikiwa kwa kufanya Road show toka kwa wataalam wa utalii ndio solution,hapo ni ulaji wa pesa tu.Kila balozi zingekuwa na afisa utalii mwenye kuwajibika na kufanya road show kwenye maeneo maalum ya kuwatafuta wateja,tungekuwa mbali sana.Hapo gharama yake tujulishe..utakimbia
ReplyDeleteNimetembelea Unguja mara tatu kuna watalii wengi kuliko huku kwetu bara na suala la utalii wapo makini sana ingawa kuliingia mushker kidogo siku zile mbaya za tindikali,any way tatizo langu ni hili..kuna tafiti zozote zimefanyika kuonyesha kwa nini utalii wetu Tanazania Bara hauziki sana ukilinganisha na vivutio vilivyopo?..Natoa hoja
ReplyDelete