Mkurugenzi
Mtendaji mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Emmanuel Humba
akisalimiana na wafanyakazi wa mfuko wakati wa hafla ya kumuaga ambapo Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (Tughe) tawi la Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF), kimemkabidhi zawadi ya sh. milioni 10 aliyekuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa mfuko huo, Emmanuel Humba kutokana na kuthamini mchango wake kabla
hajastaafu.
Mwenyekiti wa Chama
cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (Tughe) tawi la NHIF, Gabriel Ishole (kushoto)
akimkabidhi tuzo maalumu Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba kutokana na kuthamini mchango wake kabla
hajastaafu. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Emmanuel Humba akimkabidhi mke wake tuzo maalumu aliyopewa na wafanyakazi wa NHIF baada ya kustaafu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...