Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Hawa Ghasia akiwaeleza waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mafanikio ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana kote nchini ambapo umefanikiwa kwa asilimia 98%,kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh.Hawa Ghasia (hayupo pichani) na vyombo vya habari uliofanyika leo jijini Dar es salam ukilenga kueleza hatua zitakazochukuliwa na Serikali kwa wale wote waliosababisha kasoro mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana kote nchini. Picha zote na Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Pale palipokuwa na kasoro tujifunze kwa ajili ya kuboresha. Huu ni uchaguzi ambao uko karibu sana na wananchi makosa yoyote yaliyojitokeza katika uschaguzi huu yasijirudie. Mikutano ya kutathmini mafanikio na matatizo na jinsi ya kuboresha ili wananchi siku za uson wapate viongozi wanaowataka ni muhimu katika halmashauri zote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...