Mwanamuziki nguri wa muziki wa dansi
nchini, John Kitime ameibukia katika filamu na karibuni amezindua sinema
iitwayo ‘Kutakapokucha’ ambayo ina akisi watendaji wasio
waadilifu wanavyozitumia vibaya ofisi za umma na kuchangia migongano katika
jamii.
Katika filamu hiyo ambayo Kitime anacheza
kama muigizaji mkuu, akitumia jina la Nongwa, ndiye mwanakijiji pekee ambaye
nyumbani kwake kuna umemejua akijivunia televisheni wanayokuja kuiangalia na
baadhi ya wakazi wenzake kijiji na huduma za kuchaji simu anazozitoa nyumbani
kwake.
Kwa kutumia ofisi yake, anapora ardhi za
watu na mbaya zaidi anawachukia wenye mwamko kidogo wa elimu ambao binafsi
anaona hawana lolote zaidi ya kuhitaji kiti chake hali ambayo inazua migongano
na migogoro mikubwa ambayo mwisho wake ndio kinachoifanya hiyo filamu kuwa na
msisimko wa namna yake.
Filamu hiyo ambayo imeandikwa na Irene
Sanga chini ya utayarishaji wa Sylone Malalo na kuongozwa na Simon Mwakifwamba,
msambazaji mkuu ikiwa kampuni ya Proin Promotion, licha ya pia ina muigizaji
mahiri nchini, Charles Magari ‘Mzee Magari’.
Mtayarishaji wa filamu hiyo, Malalo anasema
movie hiyo inatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya filamu nchini
na anawataka wale ambao wanapenda vitu tofauti kuangalia pia inashirikisha
wasanii wa Sanaa za mapigano ‘martial arts’.
Magari ambaye anaigiza kama mtu ambaye
anataka mabadiliko kijijini hapo na kuondokana na urasimu na ukiritimba wa Mzee
Nongwa, ina waigizaji mahiri ambao pia ni walimu wa Sanaa katika Taasisi ya
Sanaa (Tasuba) ambao ni na Thabit Hudu na Mwanaidi Zambo.
Filamu hiyo ni kazi ya kwanza pia ya
mzalishaji Malalo ambaye amebobea katika utengenezaji wa picha za video,
documentary na filamu mbalimbali za kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusiana
na mambo mbalimbali ikiwa ni katika jamii na baadhi ya filamu hizo ni pamoja na
‘Zawadi’ na zingine.
NIMEIONA KITIME KAFANYA KWELI NA NI TOFAUTI NA MUVI ZETU NYINGI, HONGERA KWA WATAYARISHAJI
ReplyDelete