Mkuu
wa wilaya ya Makete Josephine Matiro ametoa agizo kwa uongozi wa kata
ya Matamba kufanya mikutano ya kuwaelewesha wananchi umuhimu wa kujenga
nyumba zao katika hali ya uimara pamoja na kupanda miti ya matunda
pembezoni mwa nyumba zao
Ametoa
agizo hilo hivi karibuni wakati alipotembelea eneo lililopata maafa ya
kuezuliwa nyumba na upepo mkali ulioambatana na mvua na kugundua kuwa
ujenzi hafifu wa nyumba zao nao umechangia kwa kiasi kikubwa hasara hiyo
"Wananchi
wanajenga nyumba hazina makoa, maeneo ni wazi hayana miti achilia mbali
ya matunda lakini hata mingine hakuna, haya maafa hayataisha, mtendaji
nakuagiza ufanye mikutano na wananchi na taarifa nipewe" alisema Matiro
katika tukio hilo hakuna vifo wala majeruhi ya watu, zaidi ya nyumba na baadhi ya vitu vilivyokuwa ndani kuharibika
Moja
ya Nyumba ya mkazi wa kijiji cha Nungu kilichopo kata ya Matamba
wilayani Makete iliyoezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua hivi
karibuni, hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa kutokana na hali hiyo
Mkuu
wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro (kulia) akiangalia moja ya
nyumba iliyobomoka kutokana na upepo huo mkali, kulia kwake ni baadhi ya
wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Makete.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...