Kulia ni Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Shinyanga Erick Chinimbaga na wa kwanza kushoto ni Afisa Fedha kutoka PSPF Makao Makuu Samweli Haule wakiwakabidhi zawadi za Krismasi watoto wenye ulemavu wa ngozi katika kituo cha Buhangija kilichopo Shinyanga  zawadi za Sikukuu ya Krismasi hapa watoto wenzao wakipokea zawadi hizo kwa niaba.  

Akikabidhi Msaada huo Afisa Fedha wa PSPF kutoka Makao Makuu alisema kwamba Mfuko wa Pensheni wa PSPF unalo lengo la kuwasaidia watoto wenye Uhitaji Maalum ili nao waweze kujisikia wapo katika jamii kama watoto wengine na kwamba kuwa hapo sio ndio kwamba wametengwa, alisisitiza kuwa Hata watakapo kuwa wakubwa wengine wataikuta PSPF na watakuwa wanachama na wengine watakuja kufanya kazi kabisa katika mfuko huo.
 Mlezi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha  Buloma Foundation kilichopo Picha ya Ndege Kibaha Bi Simphania Aidan wa kwanza kushoto akipokea Zawadi za Sikukuu ya Krismasi kwa niaba ya Msimamizi na Mwenye kituo hicho Bi.Fransisca Kyando Kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF , wa katikati ni Meneja wa PSPF Mkoa wa Pwani Msafiri Mugaka na wa kwanza kulia ni Afisa Mahusiano wa PSPF Coleta Mnyamani.  

Akikabidhi Msaada huo Meneja wa PSPF Mkoa wa Pwani Msafiri Mugaka alisema kuwa PSPF inatoa zawadi za Sikukuu ya Krismasi kwa watoto yatima ili nao washerekee vizuri na wasijisikie vibaya , aliongeza kuwa pamoja na PSPF kuwa na wanachama watu wazima lakini pia inafanya hivyo kwa watoto ili waanze kuijua PSPF wakiwa wadogo na wakiwa watu wazima waje kuikumbuka na kujiunga na Mfuko huo Bora wa Pensheni na hata kuja kufanya kazi katika Mfuko huo.

Nae Afisa Mahusiano wa PSPF kutoka Makao Makuu Coleta Mnyamani  Aliongeza neno kuwa Watoto yatima ni kama watoto wengine ambao wanahitaji kupata huduma na malezi Bora kama watoto wengine wenye wazazi au wanaolelewa bila shida yotote, alimalizia kwa kusema kuwa PSPF ipo pamoja na watoto hao wenye uhitaji na itaendelea kuwasaidia .


 Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Shinyanga wa pili kushoto  Erick Chinimbaga akimkabidhi zawadi Mmoja wa walezi wa watoto hao bwana Revocatus Robert   wa kwanza Kulia zawadi za Sikukuu ya Krismasi kwa Wasichana waliotoka katika Mazingira magumu wanaolelewa na Kituo cha Agape Mkoani shinyanga, wasichana hao walipata zawadi za Mafuta, Mbuzi, Mchele, Sabuni,Sukari pamoja na vitu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hili suala la KUWATENGA watoto wenye ulemavu wa ngozi ni baya sana. Adhari zake ni kubwa sana kijamii. Ukiwatenga wanaonekana kama sio sehemu ya jamii , sio sawa kabisa. Ni muhimu kuwarudisha kwenye familia zao, waishi na wazazi wao, wacheze na watoto wengine bila ubaguzi. Tusikimbie majukumu yetu ya kuwahakikishia ulinzi katika ngazi ya familia, jamii na hasa jeshi la Polisi tukafikiri hizi ''njia za mkato'' ndio sulihisho la kudumu. Hizi picha zinanisikitisha sana na nawaomba watanzania wenzangu tupinge kabisa hii approach.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...