Washiriki Kumi na Wanne (14) kutoka
Tanzania wajumuika na wenzao 20 kutoka nchi mbalimbali za Afrika katika
Maonyesho ya Pili Sekta ya Afya chini Uturuki. Maonyesho hayo hufanyika kila
mwaka na kwa lengo la kuendeleza mahusiano na ushirikiano katika kuboresha
Sekta ya Afya kwa nchi husika. Maonyesho ya Mwaka huu yalikuwa na washiriki
kutoka nchi 60 duniani kote. Kwa upande
wa Afrika mkutano huu ulioratibiwa na kusimamiwa na kampuni ya kuendeleza
mahusiano ya maendeleo na biashara kati ya Afrika na Uturuki iitwayo TurkaAfrica
Ltd (www.turkafrica.co.tz).
Waandaaji wa TurkAfrica wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao TUSMSIAD,na Washiriki kutoka Tanzania.
Waziri wa Afya Zanzibar
Mh. Rashid Seif Suleiman akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Afya wa Uturuki
Hon. Mehmet Müezzinoğlu. Kushoto ni Dr. Lulu Fundikira (kutoka Hopitali ya
Taifa Muhimbili) akifuatiwa na Mshauri wa mambo ya Uchumi na Maendeleo wa
Serikali ya Uturuki ambaye pia ni Raisi wa Taasisi ya Uchumi na Biashara ya
Uturuki (TUMSIAD) – Dr. Hassan Sert. Kulia ni Jumanne Simba.
Waziri wa Afya Zanzibar
Mh. Rashid Seif Suleiman akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa
sekta ya Afya wa Serikali ya Uturuki mara baada ya mazungumzo ya njia
mbalimbali za kuboresha sekta ya Afya na mahusiano kati ya Serikali ya Uturuki
na Tanzania.
Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Rashid Seif Suleiman
akifanya mazungumzo na Waziri wa Afya wa Uturuki Hon. Mehmet Müezzinoğlu.
Kushoto ni Dr. Athuman Ngenya na washiriki wengine kutoka Tanzania.
Hongereni sana Turk Africa haya ndiyo maendeleo yanayotakiwa kuletwa Tanzania na Africa kwa ujumla.
ReplyDeleteMdau - Mzalendo