Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
Wakazi wa mkoa wa Lindi wametakiwa kushikamana kwa pamoja, kufanya kazi kwa bidii na kuzitumia rasilimali zilizopo ili kujiletea maendeleo.
Rai hiyo imetolewa jana Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mitwero Stendi Kata ya Rasibura wilayani humo.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema mkoa wa Lindi umejaliwa kuwa na rasilimali nyingi ikiwa ni pamoja na zao la korosho, ardhi yenye rutuba, bahari na gesi lakini bado kuna changamoto zinazowakabili wananchi na hivyo kukwamisha maendeleo yao.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na elimu kwani baadhi ya wanafunzi wafikapo darasa la tano wanaacha shule kwa ajili ya utoro, mimba za utotoni na vijana kutokufanya kazi kwa bidii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...