WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI
UNAOTEKELEZWA NA TASAF WACHIMBA MTARO WA MAJI
KUPITIA UTARATIBU WA AJIRA YA MUDA KATIKA SHEHIA YA MPAPA,MKOA WA KUSINI
UNGUJA.
Maelfu
ya wakazi wa shehia ya Mpapa wilaya ya Kusini Unguja wanatarajiwa kunufaika na
huduma ya maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mradi wa maji
unaotekelezwa na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa
utaratibu wa ajira ya muda PWP.
Wakizungumza
katika eneo la mradi baadhi ya walengwa hao wameonyesha utayari wao katika
kuchimba mtaro huo huku wakiipongeza serikali kupitia TASAF kwa kubuni utaratibu
huo ambao wamesema licha ya kuwaongezea fedha lakini pia utapunguza kero ya
upatikanaji wa maji katika eneo lao .
Chini
ya utaratibu wa ajira za muda ,walengwa kutoka kaya maskini huibua miradi
katika eneo lao na kuitekeleza na kisha kulipwa ujira ikiwa ni mkakati wa TASAF
wa kuziongezea kaya maskini kipato kwa kukidhi mahitaji muhimu hususani katika
Nyanja za elimu,afya,lishe na uchumi, ambapo kwa mujibu wa utaratibu
asilimia 75 ya fedha ni malipo kwa
walengwa wakati asilimia 25 ni kwa ajili ununuzi wa vifaa .
Mpango
wa ajira za muda utatekelezwa nchini kote wakati wa kipindi cha hari au kipindi
kigumu kama wakati wa ukame au mafuriko kupitia Mpango wa Kunusuru kaya maskini,PSSN ambao umebuniwa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
TASAF na unatarajiwa kuhudumia kaya maskini zipatazo laki tisa na ishirini elfu
nchini kote kazi ianayotarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Marchi 2015.
ifuatazo ni
picha za baadhi ya wananchi wa shehia ya Mpapa mkoa wa Kusini Unguja
wakishiriki katika kazi ya kuchimba mtaro wa maji kupitia utaratibu wa ajira za
muda.
Baadhi
ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika shehia ya Mpapa mkoa wa
Kusini Unguja wakishiriki katika kazi ya uchimbaji wa mtaro wa maji kupitia
Mpango wa ajira za muda ambao huwawezesha walengwa kulipwa fedha .
Mtaro
wa maji uliochimbwa na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika
shehia ya Mpapa wilaya ya Kusini Unguja inayotekelezwa chini ya mpango wa ajira
za muda kupitia TASAF.
Mmoja
wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini wa TASAF katika shehia ya Mpapa
wilaya ya Kati Mkoa wa kusini Unguja akishiriki kazi ya kuchimba mtaro wa maji.
Duu! Ona nanga kiunoni.
ReplyDelete