ILIKUWA ni furaha isiyoelezeka pale Mwalimu Eliza Mhule wa Shule ya Msingi Mtoni , Manispaa ya Temeke pale alipotunukiwa shahada yake ya kwanza ya Ualimu iliyotolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kwenye Mahafali yalifanyika hivi karibuni katika mji mdogo wa Kibaha Mkoani Pwani hivi Karibuni. Katika picha Eliza yupo katika picha ya pamoja na watoto wake David Keasi (kushoto), Brian (katikati) na Aaron (kulia)
Walimu wa Shule ya Msingi Mtoni katika Manispaa ya Temeke wakiwa katika picha ya pamoja na mashaada yao ya maua muda mfupi mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Kwanza katika elimu kwenye Chuo Kikuu Huria (OUT) hivi karibuni kwenye sherehe za Mahafali zilizofanyika hivi karibuni huko Kibaha, Mkoani Pwani. Kutoka kushoto ni Mwalimu Rehema Mruma, Omari Kitwana,Anna Mwamgunda na Eliza Mhule.
Mwalimu Eliza Mhule wa Shule ya Msingi Mtoni , Manispaa ya Temeke. akivishwa shada na mwanae bada ya kulamba nondozzzz yake ya kwanza ya Ualimu iliyotolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kwenye Mahafali yalifanyika hivi karibuni katika mji mdogo wa Kibaha Mkoani Pwani
Hongereni sana walimu kwa kujikwamua kielimu
ReplyDeleteEndeleeni muweze kupaa juu zaidi. Mungu atawasaidia.
Walimu wengine igeni mfano wa walimu hao ili na nyinyi muweze kupiga hatua.