Wahitimu wa digrii ya  elimu jamii katika taaluma za maendeleo jamii wakishangilia baada ya Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya kuwatunuku katika mahafali ya 8 ya chuo hicho, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam jana.
 Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu, Rigobert Buberwa, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, Dar es Salaam. Buberwa ametunukiwa  digrii hiyo baada ya kufanikiwa kufanya utafiti unaohusu "Kuelekea modeli ya mfumo wa kompyuta wa kutunza taarifa za ardhi na mabadiliko ya umiliki wake: Nyenzo mpya ya Usimamizi wa Ardhi nchini Tanzania".
 Msuya akiongoza maandamano kutoka nje baada ya mahafali hayo kumalizika
Hali ilivyokuwa nje ya ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya mahafali kumalizika. Picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hongera sana Dawah, Mbisso, Eliwaha na Sara, kwa kutunukiwa PhD. Mdau Stklm.

    ReplyDelete
  2. Linapokujja swala la ajira, hivi hawa walamba nondo wote wanakwenda wapi?
    With unemployment rate of 11%.

    ReplyDelete
  3. karibuni mtaani tuuze vocha za simu

    ReplyDelete
  4. Unaezungumzia swala la ajira wewe ni mmoja wa wakatisha tamaa ambao wana mawazo finyu kwamba baada ya kulamba nondo lazima uajiriwe. serikalini ajira haba, kwa nini usiwape wazo la kujiajiri wenyewe? Watanzania acheni mawazo mgando hayo, ajira za kujiajiri zimejaa kibao. katika wahitimu hapo kuna architects, designers, surveyors na kadhalika. wakikusanyika wahitimu kumi wa fani mbalimbali haishindikani kufungua kampuni na kutoa huduma na ushauri na kupata kipato safi tu. Muda wa mawazo mgando umeshpita sasa jamani!!!

    ReplyDelete
  5. Kwa vyovyote vile serikali haiwezi kuepuka responsibility ya either kutengeneza ajira (formal/informal) au kuweka mazingira bora kwa ajira hizo ziweze kupatikana.Jiulize, kama serikali za mataifa yalioendelea bado wako responsible na kutengeneza mazingira ya upatikanaji wa ajira,Leo hii ukiongea kuwa nafasi za kujiajiri bongo ziko kibao sijui unaongelea ajira zipi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...