Wahitimu wa digrii ya elimu jamii katika taaluma za maendeleo jamii wakishangilia baada ya Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya kuwatunuku katika mahafali ya 8 ya chuo hicho, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu, Rigobert Buberwa, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, Dar es Salaam. Buberwa ametunukiwa digrii hiyo baada ya kufanikiwa kufanya utafiti unaohusu "Kuelekea modeli ya mfumo wa kompyuta wa kutunza taarifa za ardhi na mabadiliko ya umiliki wake: Nyenzo mpya ya Usimamizi wa Ardhi nchini Tanzania".
Msuya akiongoza maandamano kutoka nje baada ya mahafali hayo kumalizika
Hali ilivyokuwa nje ya ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya mahafali kumalizika. Picha zaidi BOFYA HAPA
Hongera sana Dawah, Mbisso, Eliwaha na Sara, kwa kutunukiwa PhD. Mdau Stklm.
ReplyDeleteLinapokujja swala la ajira, hivi hawa walamba nondo wote wanakwenda wapi?
ReplyDeleteWith unemployment rate of 11%.
karibuni mtaani tuuze vocha za simu
ReplyDeleteUnaezungumzia swala la ajira wewe ni mmoja wa wakatisha tamaa ambao wana mawazo finyu kwamba baada ya kulamba nondo lazima uajiriwe. serikalini ajira haba, kwa nini usiwape wazo la kujiajiri wenyewe? Watanzania acheni mawazo mgando hayo, ajira za kujiajiri zimejaa kibao. katika wahitimu hapo kuna architects, designers, surveyors na kadhalika. wakikusanyika wahitimu kumi wa fani mbalimbali haishindikani kufungua kampuni na kutoa huduma na ushauri na kupata kipato safi tu. Muda wa mawazo mgando umeshpita sasa jamani!!!
ReplyDeleteKwa vyovyote vile serikali haiwezi kuepuka responsibility ya either kutengeneza ajira (formal/informal) au kuweka mazingira bora kwa ajira hizo ziweze kupatikana.Jiulize, kama serikali za mataifa yalioendelea bado wako responsible na kutengeneza mazingira ya upatikanaji wa ajira,Leo hii ukiongea kuwa nafasi za kujiajiri bongo ziko kibao sijui unaongelea ajira zipi.
ReplyDelete