NA CHALILA KIBUDA WA
GLOBU YA JAMII, DAR
SHIRIKISHO la Wanafunzi wa Vyuo na Elimu ya Juu Nchini wamempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kutoa maamzi kwa wale ambao walihusika katika sakata la akaunti ya Tegeta Escrow na kwa kutengua uteuzi wake kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi , Profesa Anna Tibaijuka, kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema pamoja na kusimamishwa kazi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliackim Maswi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ,jijini Dar es Salaam, Mtendaji wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo na Elimu ya Juu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Christopher Ngubiagai, alisema maamuzi magumu ya Rais Jakaya Kikwete ni jambo la busara kwani Watanzania walikuwa wakisubiri kwa hamu maamuzi yake katika sakata la Tegeta Escrow.
Ngubiagai alisema nchi inajengwa na viongozi walio bora kuchukua maamzi pale ambapo linatokea jambo, kuweza kuchukua hatua kwa wale ambao wamekwenda tofauti ambayo ndio demokrasia imara kwa wananchi.
Aidha alisema katika hotuba ya Rais Jakaya Kikwete alipokutana na Wazee wa Jiji la Dar es Salaam Desemba 18, mwaka huu a kuwa hakuna sababu ya kutaifisha mali za muwekezaji kutokana na mfumo uliopo sasa ni ushirikiano wa Sekta Binafsi (PPP).
Wananfunzi hao waliwataka Watanzania kuwa na imani na Rais Kikwete kutokana na utendaji wake unaoonekana katika maamzi mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo na kuweza kuondokana na umasikini ambayo ndio ilani ya CCM.
Katibu Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu nchini wa Chama cha Mapindizi (CCM), Ndugu Christopher Ngubiagai akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) juu ya maamzi aliyochukua Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika sakata la Tegeta Escrow. Wengine ni Katibu wa Mkoa Dar es Salaam wa Shrikisho hilo David Zenda (Kulia), Mwenyekiti wa UWT Chuo Kikuu Huria Tawi la Ilala Evelyne Chack (kushoto).
Kitebdawili cha escrow bado ni hakijatenguliwa. Tibaijuka ametolewa lakini Tunataka kujua kiporo Muhongo, Tanesco na maswi wamehusikaje. Na wahusika wakuu wengine wote tuwajue, tujue kila mmoja kapewa fungu kiasi gani, na tujulishwe kama hizo pesa watarudisha. Na tunamuomba raisi ahakikishe wote waliohusika wanachukuliwa hatua kwa mujib wa sheria.
ReplyDeleteYa viongozi wa siasa ndio yapo uwanjani, hivi mbona sijasikia chochote kwa upande wa viongozi wa dini kuhusu upokeaji wa haya 'mapesa'? Je, tuseme hakuna uadilifu uliovunjwa kidini? Na je, kunalipi la hatua kuhusu benki iliyotumika kupitishia 'mafedhwa' hayo?
ReplyDeleteNionavyo mimi Tanzania tunakazi kubwa sana ya kubadisha maadili na hulka zetu za kijinga, uchafu wetu haupo kwa viongozi tu upo pia from our grass roots.
ReplyDeleteTunaishia kuwalaumu viongozi kila dakika wakati sisi ndio tunaowachagua ili walinde maslahi yetu madogo madogo.
Tunapata mshahara laki na nusu, familia watoto wa tano, vimada wawili na watoto kadhaa wengine. Kila siku vikao vya kila siku kwenye baa, zungusha kwa saanaaaa. Hizo pesa tunazitoa wapi budget ya karibu mil 2 kila mwezi na sisi ni wafanyakazi wa kawaida?
ofcourse lazima tumchague mtu anaye kula matawi ya juu wakati huo huo atuachie na sisi tule matawi ya chini.
Culture hii ya mtanzania wa kawaida haijaanza leo, ndo maana wabongo hatuandamani hata tukikandamizwa vipi, what for?