Na Mwandishi Wetu. Wananchi wa jiji la Dar es Salaam wamepata nafasi ya kutembelea banda la Dege Eco Village na kufahamu juu ya mradi huo wa makazi bora unaofanyika Kigamboni eneo la Ras Dege. 
Akizugumza na wananchi waliotembelea banda hilo Afisa Masoko wa Hifadhi Builders Ltd inayosimamia mradi huo Bw. Adam Jusab alisema kuwa mradi huo ni kwa ajili ya wananchi wanaohitaji makazi bora na mpaka sasa nyumba elfu mbili zimekamilika kati ya nyumba elfu saba. 
Mradi huo utajumlisha aina mbili ya nyumba yaani appartments na villas. 
Pia kutakuwa na huduma za shule, kituo cha polisi, maeneo ya burudani, kituo cha zimamoto na huduma za usafiri wa mabasi kwa uchache. 
Amesema kwamba mradi huo unatarajiwa kukamilika mwaka 2018. 
Pia aliendelea kusisitiza kwamba kama sehemu ya mazimio ya mwaka 2015 waTanzania wanashuariwa kununua nyumba zilizo kwenye makazi bora kama mradi huu wa Dege Eco Village. 
Kwa kumalizia aliwataka wale wote watakayohitaji kuwasiliana nao kufika kwenye ofisi zao zilizo mtaa wa Azikiwe Posta pembeni ya Benki ya NMB au kutembelea kwenye mtandao wa Dege Eco Village, 
www.degeecovillage.com 
au ukurasa wa facebook www.facebook.com/degeecovillage
Muuzaji kutoka Hifadhi Builders Ltd akiongea na mteja kuhusu mradi wa Dege Eco Village jijini Dar es salaam hivi karibuni
Adam Jusab, Afisa Masoko akihojiwa na waandishi wa habari hivi karibuni na kulia kwake Bwana Nyenshile, Afisa Mauzo wa Hifadhi Builders
Muuzaji kutoka hifadhi Builders Ltd akiongea na mteja na kufafanua juu ya mradi huu wa Dege Eco Village iliyopo Kigamboni.
Banda lililopo Mlimani City la Dege Eco Village jijini Dar es salaam 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kitu muhimu kwa watanzania kujihakikishia ni kuhusu usalama wa deposit mtu atakapozilipa. Iwapo Dege atajitangaza kafilisika kabla ya kukabidhi njumba mara nyingi deposit zote hupotea na kisheria Dege ni kampuni tofauti na wamiliki wake. Wakenya na wa-Rwanda wanafahamu vyema mchezo huo. Ingawa watanzania bado hayajatukuta hayo. alexbura Dar

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...