Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi sasa kutoka Mkoani Kigoma,inaeleza kuwa Abiria waliokuwa wakisafiri kwa Treni ya Reli ya Kati kutokea jijini Dar es salaam kuelekea Kigoma wamekwama wa katika Stesheni ya Uvinza mara baada ya kutokea kwa hitilafu kwenye Treni ya mizingo iliyokuwa ikitokea mkoani Kigoma kuelekea Dar es salaam.

Ripota wa Globu ya Jamii ambaye ni mmoja wa abiria hao,amezungumza na stesheni masta wa wa Uvinza na kumueleza kuwa ameshatuma wataalam kwenda eneo la tukio katika kijiji cha Rufugu ambapo ndipo Treni ya mizigo ilipopatia hitilafu za kiufundi.
Baadhi ya Abiria hao wakiwa nje ya Stesheni ya Uvinza wakijadiliana.Picha na Mdau Lulela wa Habarika24 Blog.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hiyo stesheni ni aibu tupu, tangu alipoondoka mkoloni haijawahi hata kupakwa rangi.

    ReplyDelete
  2. iko kazi, labda maintenance hela zililiwa na wajanja

    ReplyDelete
  3. Hiyo stesheni inatia aibu hata kufagia na kuiweka vizuri inangoja wawekezaji?????

    ReplyDelete
  4. Hivi sisi tukoje mbona stesheni ya Uvinza imechoka hivyo, viongozi hapo wapo mbona hawaliangalii hili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...