Afisa Masoko wa Airtel Henrick Bruno akionyesha moja kati ya
vocha za Airtel UNI255 maalum kwa vyuo vikuu nchini tayari kwa uzinduzi
jumamosi hii.
Meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando amesema “Airtel Uni 255 ni huduma pekee yakibunifu toka Airtel Maalum kwa wanafunzi wa vyuo yenye kuwapa unafuu wa kuwasiliana wawapo chuoni, sasa wanafunzi wote wa chuo wanapotaka kupata nyongeza ya vile wanavyosoma kwenye mtandao huduma hiii ndio jibu sahihi kwao kutokana na unafuu wake kwenye inteneti
· Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Shilole kupamba uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel UDSM
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel leo imebainisha kuwa mwishoni mwa wiki hii
itazindua rasmi huduma mpya maalum kwa ajili ya kutoa huduma nafuu za
mawasiliano kwa wanafunzi walioko vyuoni katika chuo kikuu cha Dar es
salaam UDSM ambapo hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo inayojulikana kama Airtel UNI 255 kwa vyuo vikuu vilivyopo Dar es salaam itafanyika katika viwanja vya Mabibo hostel
Akiongea
kuhusiana na uzinduzi wa huduma hiyo Meneja uhusiano wa Airtel Bw,
Jackson Mmbando amesema “Airtel Uni 255 ni huduma pekee yakibunifu toka
Airtel Maalum kwa wanafunzi wa vyuo yenye kuwapa unafuu wa kuwasiliana
wawapo chuoni, sasa wanafunzi wote wa chuo wanapotaka kupata nyongeza ya
vile wanavyosoma kwenye mtandao huduma hiii ndio jibu sahihi kwao
kutokana na unafuu wake kwenye inteneti, kupiga simu na hata sms. Huduma
hii tayari tumeshaizindua kwa vyuo vikuu vingine vya Dodoma, Mbeya,
Iringa, Mwanza na imeonyesha mafanikio makubwa sana kwa watumiaji
wakiwemo wanafunzi na wale wote wanaotumia huduma hii maeneo ya vyuo”
“Airtel tumeona ni vyema tuizindua hapa katika vyuo vya Dar es salaam
wiki hii siku ya Jumamosi pale mabibo hostel ambapo mbali na uzinduzi
kutakuwa na tamasha kubwa litakalopambwa na watoa burudani nguli akiwemo
Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Shilole pmaoja na DJ maarufu jiji Dj
Zero aliongeza kusema Mmbando
Nae
meneja wa huduma hiyo ya UNI 255 Anethy Muga alisema “Airtel tumeoana
hii ni huduma maalum kwa wanafunzi na ndio maana tukaona ni vyema
kuizindulia katika Hostel zao pale mabibo ambapo tunaamini wanafunzi
wengi wa chuo kikuu hapa jijini wanaifahamu na wanaishi mabibo hivyo
wanakaribishwa katika uzinduzi huo ambapo kiingilo chake ni BURE”
Burudani zitakuwa zakutosha kupitia Airtel UNI 255 siku hiyo
Kampuni
ya simu za mkononi ya airtel ilianzisha huduma ya UNI255 ili kuendana
sambamba na mkakati wao wa kusaidia vyuo vikuu nchini kutumia ipasavyo
huduma za mtandao ili kuboresha sekta ya elimu kwa lengo la kusaidia
wateja wake walioko vyuoni kufikia malengo yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...