UZINDUZI wa kitabu cha msanii
wa filamu hayati Steven Kanumba unatarajia kuandika historia kufuatia
maandalizi yaliyopangwa anasema mratibu wa tamasha hilo Mohamed Mwikongi ‘Frank’
amesema kuwa kutakuwa na mambo muhimu sana kwa ajili ya kumuenzi msanii huyo
ambaye aliitangaza Tanzania kimataifa.
“Tumepanga kufanya mambo
makubwa kwa ajili ya mwenzetu na tunataka ijengeke tabia ya kuenzi wasanii
mbalimbali, pesa za uzinduzi wa kitabu hiki utafungua Kanumba Foundation kwa
ajili ya kusaidia wanawake wajane na watoto yatima,”anasema Frank.
Frank anawakaribisha wadau wa
Kanumba kwa kufika na kujione kazi za marehemu Kanumba na kuoshuhudia wimbo
maalumu wa Marehemu Kanumba utakaoimbwa na mwanamuziki nyota Christian Bella
kwa ajili ya tukio maalum .
Kitabu cha historia ya maisha ya mwigizaji nyota
Swahilihood Hayati Steven Kanumba kinatarajiwa kuzinduliwa tarehe 10 January
2014 katika ukumbi wa Landmark Ubungo, uzinduzi huo utaambatana na maonyesho ya
kazi za marehemu Kanumba alizowahi kushiriki na kuzifanya.
Mama yake mzazi akiongea na waandishi wa habari amewashukru
wale wote ambao wamekuwa wakijaribu kufanya kazi ambazo kwa njia moja au
nyingine zinamkumbuka mwanaye ambaye aling’ara katika tasnia ya filamu
Swahilihood na kufanikiwa kutangaza Tanzania.
“Nawashukru sana watanzania na wale ambao si Watanzania
wamekuwa faraja sana kwangu, hasa pale ambapo wamekuwa wakiona umuhimu wa
kumuenzi Kanumba kwa njia tofauti tofauti, nawashukru sana, na najua kila mtu
ana mchango mkubwa si rahisi kuwataja majina maana mpo wengi,”anasema mama
Kanumba.
Kitabu hiki kinachohusu maisha ya Kanumba The Great Fallen
Tree kimeandikwa na E. Emmanuel kutoka nchini Canada na kuhaririwa nchini
Marekani na kufanyiwa uchapishaji nchini Kenya.
Uzinduzi wa kitabu utasindikizwa na Christian Bella na
Bendi ya Malaika kiingilio ni Ths. 20,000/ na utapata kitabu kimoja bure ukiingia tu mlangoni na kazi zote za Hayati
Kanumba zitapatikana siku hiyo. USIKOSE TUKIO HILI LA AINA YAKE!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...